NIDA kutoa vitambulisho vyenye saini
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa nchini Tanzania (NIDA) imekiri kwamba vitambulisho vya taifa vilivyogawiwa havina saini pande zote za nje na hivyo itautangazia umma tarehe rasmi ya kuanza kutolewa kwa Vitambulisho vilivyofanyiwa maboresho na maelekezo kuhusu Vitambulisho visivyo na saini ambavyo vimekwisha gawiwa. Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa ajili ya kuwataarifu wananchi na wadau ni kwamba vitambulisho vya Taifa vitakuwa na Saini ya Mmiliki wa Kitambulisho mbele ya Kitambulisho na Mamlaka ya Kutoa Vitambulisho vya Taifa (Mkurugenzi Mkuu) nyuma ya Kitambulisho. Taarifa hiyo imesema kuwa mamlaka hiyo kwa sasa inafanya jitihada za kurekebisha kanuni, utaratibu na muundo wa Vitambulisho ili kukidhi mahitaji ya wadau. Hata hivyo kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imesema kuwa kuweka saini juu ya Vitambulisho vya Taifa kunawezesha utambuzi ...