Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Tanzania Yapata Dili mpya Uganda La Kujenga Bomba Jingine la Gesi

Tanzania Yapata Dili mpya Uganda La Kujenga Bomba Jingine la Gesi

Picha
Baada ya Tanzania na Uganda kukubaliana mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta utekelezwe kutoka Hoima, Uganda hadi Tanga, matumaini mengine mapya yameonekana kutokana na Uganda kuweka wazi azma yake ya kujenga bomba jingine la gesi katika njia hiyohiyo kwa ajili ya biashara na Tanzania.  Licha ya kutofafanua kwa kina juu ya mpango huo, Waziri wa Maendeleo ya Nishati na Madini wa Uganda, Irene Muloni aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa Serikali ya Uganda na Tanzania bado ziko kwenye majadiliano ya kuanzisha mradi mwingine wa bomba hilo la gesi.  “Ni mpango mpya bado tunajadiliana, kuna uwezekano mkubwa wa kujenga bomba hilo lakini utekelezaji wake utaanza baada ya mradi huo wa bomba la mafuta wa sasa kukamilika,”  alisema.  Waziri Muloni aliyekuwa ameongozana na mwenyeji wake Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alitoa kauli hiyo katika mkutano wa kwanza wa jopo la watalaamu wa sekta mbalimbali waliokutana kwa mara ya kwanza kuandaa...