Upendo Kwa Wasanii Wetu Unapoanza Kuwa Kero Kwa Wasanii wa Nje
Mitandao ya kijamii imesababisha mashabiki wawe na access ya moja kwa moja na wasanii wanaowapenda. Imewasaidia kufuatilia maisha yao na kazi zao kwa ukaribu zaidi. Imewasaidia kuwapongeza wanapofanya vizuri, kuwashauri wanapoteleza, kuwakosoa wanapozingua na wengine kuitumia vibaya kwwa kuwatukana wale wasiowapenda. Kikubwa ni kwamba shabiki sasa ana full access katika career ya msanii. Kupitia mitandao ya kijamii, vita vya kishabiki vimepata uwanja wa kupigania na hicho ni kitu kinachoendelea kila siku. Lakini vipi pale ambapo mapenzi kwa wasanii wetu kwenye mitandao hiyo yanapogeuka kuwa kero kwa wengine? Mfano mzuri ni kile kinachoendelea kwa wasanii/mastaa aliopiga nao picha Diamond akiwa Marekani. Bahati tu ni kuwa Kanye West hayupo Instagram, kama angekuwepo, huenda sasa angekuwa ameshajua maneno machache ya Kiswahili kutokana na mvua ya comments kutoka kwa mashabiki wa Diamond. Lakini mtu mwenye experience hii, ni staa wa Empire, Bryshere Y. Gray maarufu kama Hakeem kwenye...