Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Sakata la Lugumi: CHADEMA Yajipanga Kumng'oa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Sakata la Lugumi: CHADEMA Yajipanga Kumng'oa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Picha
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema uzito wa Rais John Magufuli kumwajibisha Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga kutokana na kutajwa kuhusika na Kampuni ya Lugumi inayodaiwa kulitapeli Jeshi la Polisi, utasababisha waanze harakati za kumng’oa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa Rais John Magufuli hana budi kuchukua hatua haraka kumwajibisha Waziri Kitwanga kama alivyofanya kwa watumishi wengine wa umma katika operesheni ya kutumbua majipu. Waziri Kitwanga anadaiwa kuwa na hisa kwenye Kampuni ya Infosys Ips Tanzania Limited ambayo ilipewa zabuni ya kutoa huduma za kitaalamu na Kampuni ya Kimarekani ya Biometrica kuhusu uwekaji wa mashine za kielektroniki za kuchukua alama za vidole kwenye vituo 108 vya polisi.  Mkataba wa kuweka mashine hizo uliingiwa kati ya Jeshi la Polisi na Kampuni ya Lugumi Enterprises ambayo ililipwa Sh3...