Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Balozi Ombeni Sefue Amshukuru Rais Magufuli Kwa Heshima Aliyompa......Aahidi Kutoa Ushirikiano kwa Katibu Mkuu Mpya

Balozi Ombeni Sefue Amshukuru Rais Magufuli Kwa Heshima Aliyompa......Aahidi Kutoa Ushirikiano kwa Katibu Mkuu Mpya

Picha
Baada ya kudumu Ikulu kwa takribani siku 127 zikiwamo 67 tangu aongezewe muda wa mwaka moja akiwa na Serikali ya Awamu ya Tano, Balozi Ombeni Sefue ameshukuru heshima aliyopewa na Rais John Magufuli kwa muda wote aliomsaidia kutekeleza majukumu yake ya ukatibu mkuu kiongozi na kueleza kuwa Serikali ya sasa ni ya mabadiliko.  Wakati Sefue akiondoka, mhandisi John Kijazi amepokea kijiti cha ukuu wa utumishi serikalini na kuahidi kuwa atafuatilia mazingira ya watumishi wote pamoja na mazingira yao, ili kurekebisha panapohitajika kwa lengo la kuongeza uwajibikaji na tija kwa wananchi. Akizungumza muda mfupi baada ya kuapishwa kwa mrithi wake, licha ya kumshukuru Rais, Balozi Sefue aliwataka watendaji wote serikalini kumpa ushirikiano wa kutosha Balozi Kijazi ili kuleta ufanisi kwenye huduma za umma. “Namshukuru Rais kwa kuniamini kwa kipindi chote nilichodumu naye. Ni heshima kubwa kuwatumikia Watanzania pamoja naye. Nitampa ushirikiano wowote atakaouhitaji katibu mkuu kiongo...