Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya KILIMO BORA CHA ALIZETI

KILIMO BORA CHA ALIZETI

Picha
Alizeti ni kati ya mazao yanayotoa mbegu za mafuta. Hutoa mafuta kati ya asilimia 45-55 na mashudu yake ni chalula cha mifugo. Alizeti huvumilia ukame na hulimwa kwa ajili ya biashara na matumizi ya nyumbani. Wakulima huvuna kiasi kidogo, kati ya gunia 3-5 kwa ekari. Hivyo kwa mavuno mengi na bora, mkulima anashauriwa kuzingatia mambo yafuatayo:- 1. KUANDAA SHAMBA. Unashauriwa kutayarisha shamba lako mapema kwa kukatua ardhi na kulainisha vizuri. Samadi yaweza kuchanganywa vizuri na udongo wakati wa kuandaa shamba. 2. WAKATI WA KUPANDA. Maeneo yenye mvua nyingi alizeti huanza kupandwa mwishoni mwa mwezi Januari mpaka katikati ya mwezi Februari. Maeneo yenye mvua kidogo alizeti hupandwa mwezi Desemba hadi Januari. 3. KIASI CHA MBEGU NA UPANDAJI. Kiasi cha kilo 3-4 za mbegu zinatosha kupanda eneo la ekari moja. Panda mbegu 3-4 ktk kila shimo kwa nafasi ya sentimita 75 kutoka mstari hadi mstari na sentimita 30 kutoka shimo hadi shimo. Shimo la mbegu liwe na kina cha sentimita 2.5-5...