Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya MSD Yaigeuzia Kibao Muhimbili Kuhusu Kuhusu Utata wa Dawa Uliobuliwa na CAG

MSD Yaigeuzia Kibao Muhimbili Kuhusu Kuhusu Utata wa Dawa Uliobuliwa na CAG

Picha
Sakata la upotevu wa vifaatiba na dawa kutoka Bohari ya Dawa (MSD) kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kipindi cha miaka minne limeingia katika sura mpya baada ya MSD kuigeuzia kibao hospitali hiyo, huku ikitoa ushahidi wa ankara 23 zilizotumika kupelekea vifaa hivyo kwa kipindi cha miaka minne.  Ripoti iliyotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Juma Assad inaonyesha ukaguzi ulifanyika Muhimbili, huku rekodi zikionyesha kwamba hospitali hiyo ilikuwa ikiagiza mzigo kutoka MSD, lakini hazionyeshi kupokea vifaa hivyo tangu mwaka 2012/14. Kwa kutumia vielelezo vya nyaraka hizo mbele ya vyombo vya habari jana, MSD ilitoa ufafanuzi kuwa haihusiki katika upotevu huo kwani iliwasilisha MNH vifaatiba na dawa zenye thamani ya Sh2.6 bilioni na kupokewa stoo kwa nyakati tofauti kwa kipindi cha miaka minne.  Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Lauren Bwanakunu alisema hati za CAG, zinaonyesha kuwa MSD haina tatizo lolote.  “Ankara hizo...