Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Kuendelea mgogoro wa Burundi licha juhudi za kisiasa

Kuendelea mgogoro wa Burundi licha juhudi za kisiasa

Picha
Katika hali ambayo Umoja wa Afrika umeimarisha kamati ya usuluhishi nchini Burundi kwa minajili ya kuhitimisha mgogoro wa kisiasa unaoikabili nchi hiyo, bado machafuko yanatajwa kuendelea katika nchi hiyo mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.Duru za kipolisi jijini Bujumbura zimearifu kuwa, watu waliokuwa na silaha wamefanya mashambulizi kaskazini mwa nchi hiyo. Katika shambulio hilo, watu 10 wamejeruhiwa huku wengine hali zao zikiwa mbaya sana.Hayo yanajiri katika hali ambayo wiki iliyopita Benjamin William Mkapa, rais wa zamani wa Tanzania aliteuliwa kuwa mkuu wa timu ya upatanishi itakayotumwa na Umoja wa Afrika kwenda nchini Burundi katika jitihada za kuupatia ufumbuzi mgogoro huo. Kuchaguliwa Mkapa kumefanyika baada ya safari ya ujumbe wa Umoja wa Afrika iliyowahusisha marais kadhaa wa Kiafrika chini ya uongozi wa Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini kwa ajili ya kumshawishi Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi aruhusu kutumwa nchini humo waangalizi wa umoja huo. Kabla ya hapo Rais...