Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Serikali Kuajiri Askari Wapya 3700....... Askari 7000 na Wakaguzi 1300 Watapandishwa Vyeo

Serikali Kuajiri Askari Wapya 3700....... Askari 7000 na Wakaguzi 1300 Watapandishwa Vyeo

Picha
Serikali  inatarajia kumwaga ajira kwa askari  katika mwaka ujao wa fedha.Taarifa juu ya ajira hizo, zilitolewa jana bungeni  na  waziri  mwenye dhamana. Akiwasilisha Makadirio ya Mapato ya Matumizi ya Wizara yake kwa mwaka 2016/17 kuhusu ajira za askari, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga alisema wataajiriwa askari wapya 3,700 katika mwaka wa fedha 2016/17. Waziri Kitwanga alisema mbali ya kuajiri askari hao, pia watawapandisha vyeo askari 7,140, wakaguzi 1,325 na maofisa 991. Alisema katika mwaka 2015/16, jumla ya askari polisi wapya 3,882 waliajiriwa, na askari wakaguzi na maofisa 4,065 wa vyeo mbalimbali walipandishwa vyeo kwa kufuata utaratibu wa ajira. “Aidha, serikali imeendelea kuhuisha viwango vya mishahara na posho mbalimbali, ikiwemo posho ya chakula ambayo iliongezwa kutoka Sh 180,000 hadi kufikia Sh 300,000 kwa mwezi,” alieleza Waziri Kitwanga. Alisema katika mwaka ujao wa fedha, Jeshi la Polisi litaongeza umakini ...