Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya kinaweza kuikuta Barcelona msimu huu

Kilichoikuta Mallorca msimu wa 1998/99 kwa Van Gaal, kinaweza kuikuta Barcelona msimu huu

Picha
Barcelona walionekana wanaelekea kutwaa ubingwa wa pili mfululizo wa La Liga siku kadhaa tu nyuma, lakini kuanguka kwa kiwango chao kumewafanya sasa wawe sawa kwa pointi na Atletico Madrid kwenye kiti cha uongozi wa ligi, pointi moja nyuma ya Real Madrid.    Mnamo March 20, kikosi cha Luis Enrique kikiwa kinaongoza 2-0 vs Villareal, kikaruhusu wapinzani wao warudi mchezoni na kusawazisha magoli yote katika mchezo uliopigwa katika dimba la Estadio El Madrigal. Wakati huo ilionekana ni kosa dogo Barca wamefanya na halitokuwa na athari kubwa katika mbio zao za ubingwa. Hakuna ambaye aliyapa umuhimu mkubwa matokeo ya mechi ile. Mechi zilizofuatia mbili za Wakatalunya hazikuwa nyepesi, walikuwa wanakutana na Real Madrid CampNou, kisha kufunga safari kwenda Estadio de Anoeta kucheza vs Real Sociedad.    Hata hivyo, kila mtu alitabiri Barca wangewaadhibu vijana wa Zinedine Zidane, na ilikuwa muda wa muafaka kwa Luis Enrique kulipa kisasi dhidi ya Real Sociedad baada y...