HAYA NDIO MAAMUZI YA RUFAA YA TIGO DHIDI YA HUKUMU YA KUWALIPA AY NA MWANA FA
AY akiwa na mwanasheria wake Alberto Msando nje ya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam Mahakama Kuu ya Tanzania leo imesikiliza mapingamizi ya awali ya maombi ya rufaa yaliyowasilishwa na kampuni ya mawasiliano nchini Tigo dhidi ya hukumu iliyotolewa na mahakama ya wilaya ya Ilala, April 11 mwaka huu ya kutakiwa kuwalipa AY na Mwana FA shilingi bilioni 2.18 kama fidia ya kutumia nyimbo zao bila ridhaa yao. Mapingamizi hayo matatu yamewasilisishwa na Mwana FA na AY kupitia mwanasheria wao, Alberto Msando. Miaka minne nyuma, wasanii hao wawili walifungua kesi ya madai dhidi ya kampuni ya Tigo baada ya kutumia nyimbo zao ‘Dakika Moja’ na ‘Usije Mjini’ kama miito ya simu kwa wateja wake bila kuwa na mikataba nao. Ijumaa hii, Mhe. Isaya Arufani ambaye ni Naibu Msajili wa Mahakama ya Tanzania alisikiliza utetezi kutoka kwa mawakili wa pande hizo mbili. Mwana FA na AY walikuwepo pia mahakamani hapo. Mhe. Arufani ametaija June 27 kuwa siku ya kusikilizwa kwa maamuzi...