Wasiwasi kuhusiana na kutiwa nguvuni wapinzani wa serikali ya DRC
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema anatiwa wasiwasi na kutiwa nguvuni baadhi ya wapinzani wa kisiasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na mbinyo wa kisiasa unaoshuhudiwa nchini humo.Idadi kadhaa ya wanaharakati wa kisiasa wa eneo la mashariki mwa Kongo DR wamehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa tuhuma za kuchochea uasi dhidi ya serikali. Aidha Mahakama Kuu ya mji wa Goma ulioko kwenye mpaka wa mashariki wa nchi hiyo imewahukumu adhabu ya kifungo cha miaka miwili jela wanaharakati sita wa Harakati ya Wananchi ya Mapambano kwa ajili ya Mabadiliko.Ilidaiwa mahakamani na upande wa serikali ya Kinshasa kuwa watu hao ni waasi. Itakumbukwa kuwa wapinzani na wanaharakati wa asasi za kiraia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo walitoa wito kwa wananchi kushiriki kwenye maandamano ya kupinga serikali ambayo yalikuwa yamepangwa kufanyika tarehe 16 ya mwezi huu wa Februari katika mji mkuu wa nchi hiyo Kinshasa.Tarehe 16 Februari, inaadhimishwa kukumbuka umwagaji damu wa...