Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Rais Magufuli Awataka Makandarasi Wazawa Kuwa Wazalendo

Rais Magufuli Awataka Makandarasi Wazawa Kuwa Wazalendo

Picha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka wakandarasi kote nchini kufanya kazi kwa kutanguliza maslai ya taifa, badala ya kutaka kupata faida kubwa kupita kiasi kutoka kwenye zabuni za miradi ya ujenzi wanayopata kutoka serikalini. Dkt. Magufuli amesema hayo leo tarehe 26 Mei, 2016 alipokuwa akifungua mkutano wa mashauriano wa bodi ya usajili wa wakandarasi kwa mwaka 2016 unaofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es salaam. Rais Magufuli amesema serikali yake ipo tayari kuwapa kipaumbele wakandarasi wa Tanzania pale inapotangaza zabuni za miradi ya ujenzi, lakini amewataka kujirekebisha kwa kupanga viwango vinavyostahili vya gharama za ujenzi wa miradi hiyo ambavyo serikali itaridhika. “Nawatolea mfano, idara ya mahakama imetangaza kujenga mahakama za mwanzo na za wilaya, kwenye bajeti wana shilingi bilioni 24, makadirio ya kitaalamu yanaonesha kila jengo lisizidi shilingi milioni 200, wakandarasi wazalendo walipoo...