Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Mwakyembe Ataka Mishahara na Posho za Wabunge wa UKAWA Zifutwe.........Keissy Awafananisha na Watumishi HEWA

Mwakyembe Ataka Mishahara na Posho za Wabunge wa UKAWA Zifutwe.........Keissy Awafananisha na Watumishi HEWA

Picha
WABUNGE wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ambao wamekuwa wakiingia bungeni kusaini posho na kuondoka, wako hatarini kufutiwa posho kama wataendelea kususa vikao vya Bunge kama walivyotangaza. Hali hiyo inatokana na hoja zaidi ya mbili zilizowasilishwa kwa Spika wa Bunge kwa njia ya Mwongozo huku moja ikiwasilishwa na Waziri mwenye dhamana ya Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe, zikikusudia kutaka Bunge kufuta posho za wabunge hao. Akizungumza jana bungeni baada ya kuruhusiwa na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson, Dk Mwakyembe akitumia ibara za Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 na Kanuni za Kudumu za Bunge, alitaka uongozi wa Bunge kutazama upya kama wabunge hao wanastahili kulipwa posho. Dk Mwakyembe, kwanza alitumia Ibara ya 26 ibara ndogo ya kwanza na ibara ndogo ya pili ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo aliinukuu;  “Kila mtu ana wajibu wa kufuata na kutii Katiba hii na sheria za Jamhuri ya Muungano. Kila mtu ana haki, kwa kufuata utaratibu u...