Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako Awasimamisha Kazi vigogo watatu taasisi ya elimu
JOYCE Ndalichako, Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, amewasimamisha kazi watumishi watatu wa Bodi ya Taasisi ya Elimu nchini (TET) kwa kushindwa kusimamia sheria ya manunuzi na kazi ya uchapaji wa vitabu ili kupisha uchunguzi Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Maimuna Tarishi ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, amesema watumishi hao hawakutekeleza majukumu yao ipasavyo na kuruhusu vitabu hivyo kuchapishwa vikiwa na mapungufu. “Mnamo tarehe 22 Januari mwaka 2016 bodi hiyo ilishauriwa kusitisha uchapaji wa vitabu uliokuwa ukifanywa na kampuni ya Yukos Enterprises Ltd baada ya kubainika kuwa na mapungufu, lakini haikusitisha,” amesema Tarishi na kuongeza. “Serikali iliamua kusitisha uchapishaji wa vitabu hivyo ili isiendelee kupokea vitabu vyenye mapungufu, hata hivyo taasisi ya elimu haikusitisha uchapishaji wa vitabu hivyo, badala yake kampuni hiyo ilichapisha vitabu vyote ilivyopangiw...