Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Serikali Yanasa Kilo 34

Serikali Yanasa Kilo 34,000,000 za Sukari Mafichoni

Picha
Shehena ya sukari ya kilo milioni 34 zilizokuwa zimefichwa kwenye maghala ya wafanyabiashara watatu Kilimanjaro imekamatwa na vyombo vya usalama, na serikali mkoani humo imetangaza kuiuza kwa wananchi kuanzia jana kwa bei elekezi ya Sh. 1,800. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Mecki Sadiki alithibitisha jana kukamatwa kwa shehena hiyo, baada ya makachero wanaoongoza timu maalumu ya ukaguzi wa maghala ya wafanyabiashara na mawakala wa sukari kubaini kufichwa kwa bidhaa hiyo. “Tumefanya ukaguzi katika maghala 45 na katika harakati hizo tumenasa tani 34 (kilo milioni 34) za sukari iliyokuwa imefichwa,"  alisema. "Katika zoezi hilo kuna mfanyabiashara mmoja mkubwa, yeye alikutwa na tani 31.33 lakini alikuwa akiiuza, isipokuwa bado tumewapa kazi Mamlaka ya Mapato (TRA) ichunguze kama imehodhiwa isivyo halali,”  alisema Sadiki. Kiasi cha sukari iliyobakia, alisema Mkuu wa M koa huyo, kilikamatwa kwa wafanyabiashara wengine wawili, ambao walikuwa na tani nne kasoro,...