Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Exclusive… DJ Maarufu Dar Adai: Nimezaa na Mama Diamond Platnumz

Exclusive… DJ Maarufu Dar Adai: Nimezaa na Mama Diamond Platnumz

Picha
Kumekuwepo na usiri juu ya baba wa mdogo wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Esma Platnumz lakini huenda utata ukafika mwisho baada ya aliyekuwa DJ maarufu jijini Dar kuibuka na kudai kuwa ndiye aliyemzaa mtoto huyo na mama Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ akimpinga na kuamua kumuweka wazi baba halali wa Esma.  ILIKUWAJE?   Mapema wiki hii, mtu mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Jerry Kato mkazi wa Boko jijini Dar, alipiga simu kwenye chumba cha habari cha gazeti hili na kueleza kuwa, ana jambo linaloutesa moyo wake na kwamba amekuwa akitafuta kuwasiliana na Magazeti ya Global kwa muda mrefu hivyo angependa kukutana na mwandishi wetu ili atoe lililoukamata moyo wake.  WAKATUNA BOKO   Baada ya kufanyika mawasiliano, mwandishi wetu na Jerry walikutana na jamaa huyo huko Boko, nje kidogo ya Jiji la Dar ambapo alifunguka kuwa, yeye ndiye baba mzazi wa Esma Platnumz ila anashangaa mama wa mtoto huyo amekuwa akikwepa kumtambulisha....