Mapato Hospitalini Yanuka Ufisadi.....Vifaa vya Kielektroniki Vya Kuyakusanya Vyaiduwaza Serikali
Ufungaji wa vifaa vya kielektroniki katika hospitali za Serikali katika mikoa mbalimbali, umeibua fukuto la ufisadi mkubwa, uliokuwa ukifanywa katika makusanyo ya fedha wanazolipa wagonjwa kwa ajili ya huduma. Akizungumza bungeni mjini Dodoma jana katika kipindi cha maswali na majibu, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo, alisema tangu mfumo huo wa kielektroniki uanze kutumika katika hospitali nyingi nchini, mapato yameongezeka. Jafo alisema mafanikio hayo ya ukusanyaji wa mapato kwa mfumo wa elektroniki, yamesababisha katika sekta ya afya kwa sasa ajenda kuu iwe kuongezea mapato ya hospitali zote nchini, kuendane na utoaji wa huduma bora. Hospitali ya Rufaa Mbeya Akitoa mfano wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Jafo alisema kabla ya kufungwa kwa vifaa hivyo, ilikuwa ikikusanya Sh milioni 70 kwa mwezi, lakini baada ya kufungwa vifaa hivyo, mapato yameongezeka zaidi ya mara saba na kufikia Sh milioni 500 kwa mwe...