Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya SIMBA YAITUNGUA MBEYA CITY KWA MARA YA KWANZA TAIFA NA KUREJEA KILELENI MWA VPL

SIMBA YAITUNGUA MBEYA CITY KWA MARA YA KWANZA TAIFA NA KUREJEA KILELENI MWA VPL

Picha
Wachezaji wa Simba Awadh Juma (ushoto) na Ibrahim Ajib (kulia) wakishangilia goli la kwanza lilifungwa na Danny Lyanga Ushindi wa magoli 2-0 iliyoupata leo timu ya Simba SC dhidi ya Mbeya City kwenye uwanja wa taifa ni ushindi wa kwanza wa ‘Wekundu hao wa Msimbazi dhidi ya Mbeya Mbeya City kwenye uwanja wa taifa. Simba ilikuwa haijawahi kuifunga City kwenye uwanja wa taifa tangu timu hiyo ilivyopanda kucheza ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara. Mechi ya kwanza Simba ilitoka sare ya kufungana kwa bao 2-2 dhidi ya Mbeya City kisha ikakubali kichapo cha goli 2-1 kwenye mchezo wa pili kabla ya leo kuikandamiza kwa mabao 2-0. Magoli ya Simba kwenye mchezo wa leo yamefungwa na Danny Lyanga ambaye aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya mshambuliaji wa kiganda Hamisi Kiiza kisha Ibrahim Ajib akatupia bao la pili baada ya kuongezwa dakika moja zikiwa dakika 90 zimemalizika. Rekodi na matukio muhimu unayotakiwa kujua Simba inafanikiwa kurejea kileleni mwa VPL kwa mara pili msimu h...