Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Huyu Sallam Kumbe ndio Kila Kitu Kwa Mwanamuziki Diamond..Mfahamu Hapa

Huyu Sallam Kumbe ndio Kila Kitu Kwa Mwanamuziki Diamond..Mfahamu Hapa

Picha
DIAMOND Platinumz ni mwanamuziki mkubwa Afrika, inatajwa kuwa msanii huyo ana timu nzuri nyuma yake ambayo imemwezesha kupata mafanikio mengi makubwa.  Ukiachana na Said Fella na Babu Tale, kuna mtu anaitwa Sallam ambaye inaaminika ni mmoja wa watu muhimu katika menejimenti ya Diamond. Sifa yake kubwa inayotajwa kuwa ni mzuri kutengeneza ‘connection’ nyingi zilizompaisha Diamond kimataifa.  Mashabiki na wadau wengi hawamfahamu kiundani, siku za hivi karibuni staa mwingine wa Bongo Fleva, AY alimtaja Sallam kuwa meneja wake. Sallam amezungumza na gazeti hili na kufunguka mengi:  Championi: Unajulikana kwa jina la Sallam, umetokea wapi na ulianzaje umeneja?   Sallam: Naitwa Sallam Sharaf, nilizaliwa Dar na nikasomea Morogoro. Muziki nilianza muda mrefu tangu nikiwa Shule ya Forest, Morogoro. Tulikuwa na kundi letu la Watukutu, tulikuwa tuna-rap, liliundwa na Puzzo, Swedi na mimi nikijiita OG.  Watukutu ilikuwa ikileta ushindani wa wasanii wa Dar...