Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Wahadhiri UDOM Wataja Kiini cha Mgomo Kilichosababisha Wanafunzi 7802 Warudishwe Nyumbani

Wahadhiri UDOM Wataja Kiini cha Mgomo Kilichosababisha Wanafunzi 7802 Warudishwe Nyumbani

Picha
JUMUIYA ya Wanataaluma ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOMASA) imesema kilichotokea si walimu kugoma kufundisha programu ya Stashahada Maalumu ya Elimu, Sayansi, Hisabati na Tehama, bali tatizo ni kutoelewana na Menejimenti ya chuo kutokana na mazingira mabovu ya uendeshaji wa programu hiyo chuoni hapo. Aidha, imelaani kitendo cha wanafunzi 7,802 wa Programu Maalumu ya Ualimu wa Msingi na Sekondari, waliorudishwa nyumbani bila kupewa muda wa kutosha kujiandaa kwa kuzingatia umri wao na mazingira waliyokuwa wanaishi, hali inayofanya wazagae mitaani huku wakiwa hawana pa kwenda. Hayo yako kwenye tamko lililotolewa jana na Katibu wa jumuiya hiyo, Lameck Thomas, ambalo lilieleza kuwa lawama zimekuwa zikitupwa kwa walimu kutokana na taarifa hizo kutolewa na upande mmoja, ambao ni Menejimenti ya chuo kwenda serikalini bila kuwepo na taarifa yoyote kutoka kwa walimu kupitia jumuiya yao. Thomas alisema si kweli kama walimu waligoma kufundisha lakini tatizo kubwa ni kutoelewana kati ya walimu n...