Bungeni: Mbunge aibana serikali Kuhusu fedha za Maendeleo
Mbunge wa Kavuu, Dk Prudenciana Kikwembe (CCM) ameitaka Serikali kueleza ni lini itatoa fedha kwa ajili ya shughuli za maendeleo kwa wakati. Dk Kikwembe akiuliza swali la nyongeza bungeni, alisema mara nyingi fedha za maendeleo zimekuwa zikipelekwa katika maeneo husika kwa kuchelewa na hivyo kuchelewesha miradi mingi. “Ni lini fedha za utekelezaji wa shughuli za maendeleo zitatolewa kwa wakati na fedha zinapochelewa na kutolewa mwishoni mwa mwaka wa fedha, fedha hizo huwa zinaenda wapi?” Alihoji Dk Kikwembe. Akijibu swali hilo, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jaffo alikiri kuwa miradi mingi ya maendeleo imekuwa ikisuasua kutokana na ukosefu wa fedha. Hata hivyo alisema, kutokana na jitihada zilizopo za kukusanya mapato ya Serikali, tayari baadhi ya miradi iliyokwama imeshaanza kutekelezwa na anaamini miradi yote iliyokuwa imekwama itatekelezwa kabla ya kumalizika kwa mwaka huu wa fedha. Awali, katika swali la msin...