DI MARIA AMPA BIBI YAKE GOLI LA ARGENTINA
Argentina wameinyuka Chile mabao 2-1 katika mchezo wao wa kwanza wa kundi D wa michuano ya Copa America Centenario uliochezwa katika uwanja wa Levi huko Clara, Calif. Argentina maarufu kwa jina la ‘La Albiceleste’ walikuwa bila ya nyota wao Lionel Messi kutokana kuendelea kuuguza majeraha yake ya mgongo aliyopata katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Honduras uliochezwa Mei 27. Baada ya kutokuanza vizuri nusu ya kwanza, Argentina walikuja kwa kasi ya aina yake, ambapo mnamo dakika ya 51, Angel Di Maria alifunga goli maridhawa baada ya kupata pasi nzuri kutoka kwa Eva Banega. Baadaye Argentina waliongeza bao la pili dakika ya 59 lililofungwa na Eva Banega baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Angel Di Maria. Bao pekee la Chile lilifungwa kwa kichwa na Jose Fuenzalida dakika ya 90 kutokana na pasi nzuri ya Fabian Orellana na kufanya matokeo kuwa 2-1. Kwa sasa Argentina na Panama wanaoongoza kundi D wote wakiwa na alama tatu na magoli 2 ya kufungwa na moja la kufungwa huk...