Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Mbowe aonya utumbuaji majipu

Mbowe aonya utumbuaji majipu

Picha
Mwenyekiti wa Chadema ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), amekemea kile alichokiita “fukuza fukuza” ya watumishi wa umma bila kufuata taratibu. Kauli ya Mbowe imekuja wakati Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli, ikiwa katika kampeni ya kufukuza na kusimamisha watumishi wa umma wanaotuhumiwa kuhusika katika ubadhirifu, wizi, uzembe na njama za kuhujumu mapato. Operesheni hiyo inafanyika kwa kuwasimamisha kazi watumishi hao huku uchunguzi ukiagizwa kufanywa wakati tuhuma zao zikiwa zimeshatajwa hadharani. Tayari watumishi zaidi ya 160 wameshasimamishwa au kufukuzwa kazi tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani. Kati yao, tayari wachache wamefikishwa mahakamani. Mbowe alisema ufukuzaji watumishi wa umma bila ya kufuata taratibu hautakiwi na kuwataka viongozi wa dini kukemea mwenendo huo. Alitoa kauli hiyo mbele ya Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Fredrick Shoo katika ibada maalumu ili...