Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Watu Watatu Wanaosadikiwa Kuwa Majambazi Wauawa Katika Jaribio La Uhalifu Wilayani Chunya Mkoani Mbeya

Watu Watatu Wanaosadikiwa Kuwa Majambazi Wauawa Katika Jaribio La Uhalifu Wilayani Chunya Mkoani Mbeya

Picha
 JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA. Mnamo tarehe 27.04.2016 majira ya saa 20:00 usiku huko katika Kijiji na Kata ya Matundasi, Tarafa ya Kiwanja, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya, watu watatu wanaosadikiwa kuwa majambazi waliuawa katika majibizano ya risasi na askari polisi wakiwa katika harakati za kufanya uhalifu kwenye duka bia la jumla mali ya bwana HAMIS mkazi wa Matundasi. Inadaiwa kuwa majambazi hao wapatao watano walikuwa wakitumia pikipiki mbili huku pikipiki moja ikibeba majambazi watatu na nyingine majambazi wawili huku wakiwa na silaha aina ya SMG yenye namba 1996 AFU 1120 na risasi 26 kwenye magazine walitaka kufanya uhalifu kwenye duka la jumla la kuuza bia mali ya HAMISI. Kutokana na taarifa za siri/intelejensia, Jeshi la Polisi lilijipanga kukabiliana na majambazi hao na katika majibizano ya risasi, jambazi mmoja ambaye alikuwa na silaha aina ya SMG yenye namba 1996 AFU 1120, risasi 26 kwenye magazine aliuawa baada ya kujeruhiwa kwa kupigwa risasi tumboni na mguuni ...