Kudharau Iran ni kosa ambalo linaweza kugharimu sana. | T MEDIA NEWS
Mwanajeshi wa zamani wa Marekani anasema kufikiri Marekani inaweza kuvamia Iran kirahisi ni wazimu. Matt Bracken, mwanajeshi wa zamani wa kikosi maalum cha US Navy SEAL, amesema: “Irani hawana shida kufa kwa ajili ya malengo yao, hasa kama sisi ndio tunaovamia. Yeyote anayefikiri kuwa Marekani ina ubora wa kiteknolojia, na kwamba wanajeshi wa Marekani (Marines) ni wagumu zaidi kuliko Walinzi wa Mapinduzi ya Iran (IRGC), kwa kweli anafanya wazimu. Wanachoweza kufanya ni kuwaacha Wamarekani waingie. Watazima rada, watazima mifumo ya ulinzi. Kisha watafunga mtego.” Kauli nzito imetolewa na Matt Bracken, mwanajeshi wa zamani wa kikosi maalum cha US Navy SEAL mtu anayeelewa vizuri uwanja wa vita. Anasema wazi kabisa: Kufikiri Marekani inaweza tu kuingia Iran na kushinda kwa urahisi ni kosa kubwa la kimkakati. Kwa nini? Kwanza, Iran si taifa la kawaida. Hii ni nchi ambayo imejenga mfumo wake wa kijeshi kwa miongo kadhaa, ikiwa na lengo moja kujilinda dhidi ya uvamizi mkubwa wa nje. Pil...