Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Sheria ya Mahakama ya Mafisadi Yatinga Rasmi Bungeni

Sheria ya Mahakama ya Mafisadi Yatinga Rasmi Bungeni

Picha
Serikali imewasilisha miswada miwili ya marekebisho ya sheria mbalimbali ya mwaka 2016 ikiwamo ya kuanzishwa kwa Mahakama Maalumu ya Rushwa. Watakaokutwa na hatia ya makosa ya rushwa au uhujumu uchumi, watafungwa kifungo kisichopungua miaka 20 na kisichozidi miaka 30. Kuanzishwa kwa mahakama hiyo ni kutimiza ilani ya CCM na ahadi ya Rais John Magufuli kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka jana kuwa ataianzisha ili kushughulika na mafisadi pamoja na wahujumu uchumi. Kwa mujibu wa muswada huo, mahakama hiyo inaanzishwa katika marekebisho ya Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura ya 200 yatakayo fanyika katika Kifungu cha 3.   “Lengo la marekebisho hayo ni kuanzisha Divisheni ya Mahakama Kuu ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi itakayokuwa na mamlaka ya kusikiliza na kuamua mashauri yanayohusiana na makosa ya rushwa na uhujumu uchumi, ambayo itakuwa na mamlaka ya kusikiliza mashauri yenye thamani isiyopungua Sh1 bilioni,”  unaeleza muswada huo uliowasilishwa kwa mara ya...