Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Mbunge: Pinda alitaka kuchomokea dirishani Baada ya Kutoswa na CCM

Mbunge: Pinda alitaka kuchomokea dirishani Baada ya Kutoswa na CCM

Picha
Mbunge wa Ulanga, Gudluck Mlinga (CCM), amesema Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda, alitaka kuchomokea dirishani baada ya kutoswa katika uteuzi wa urais ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana. Mlinga ambaye pia ni mtoto wa marehemu, Selina Kombani, alitoa kauli hiyo juzi jioni, wakati akichangia bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Alisema baada ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuhamia upinzani na wenzake, Pinda naye alitaka kuwafuata, lakini akashtuka na kubaki CCM. “Yule mwingine alituzingua tukampiga chini akaenda upinzani, Pinda naye mwaka jana alitetereka, tukamtosa akataka kuchomokea dirishani… akashtukia akabaki, kwahiyo CCM hatufanyi mambo kwa kuambiwa kama wanavyofanya upinzani,”  alisema. Kauli ya Mlinga ilionekana kumkera Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ali Keissy (CCM) ambaye aliomba kutoa taarifa: “Mheshimiwa mwenyekiti nampa taarifa mzungumzaji, amemvunjia heshima Pinda kwa kusema alitokea dirishani, afute kau...