Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya UVCCM Wamtaka Fredrick Sumaye Amwache Rais Magufuli Afanye Kazi Yake

UVCCM Wamtaka Fredrick Sumaye Amwache Rais Magufuli Afanye Kazi Yake

Picha
Umoja wa vijana wa Chama cha mapinduzi umesema Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye hana vigezo wala sifa zozote zinazoweza kumfanya awe na uwezo wa kumkosoa Rais Dk John Magufuli katika uendeshaji wa serikali na masuala ya utawala. Sumaye ametakiwa amuache Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk Magufuli ili atimize majukumu yake kwa sababu alipewa dhamana ya kuwa Waziri mkuu lakini hakufikia hata theluthi ya utendaji unaofanyika sasa. Msimamo huo umetolewa jana na Kaimu katibu mkuu wa uvccm shaka hamdu shaka alipokuwa akizungumza na wanachama wa ccm wa kata mbili za kwandele na mbichi jimbo la Rombo mkoani kilimanjaro. Shaka alisema anachokifanya Sumaye na baadhi ya wanasiasa muflis wanaojaribu kukosoa utendaji katika utawala wa serikali ya awamu ya tano ni kutaka nao wasikike wakidhani yale walioyafanya wakati wakiwa madarakani wananchi wameyasahau. Alisema kama yupo waziri mkuu ambaye ameonyesha udhaifu katika utendaji na usimamizi wa serikaki huku akishindwa kumsaidia Rai...