Waziri Mkuu Majaliwa atembelewa na Waziri Viwanda wa Singapore Bungeni Mjini Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungao wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa amewakaribisha wafanya biashara kutoka nchini Singapore kuja kuwekeza nchini Tanzania kutokana na fursa zilizopo nchini katika sekta mbalimbali za maendeleo. Waziri Mkuu ametoa rai hiyo leo mjini Dododma alipokuwa akiongea na Ujumbe wa Singapore ulioongozwa na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Biashara na Viwanda Mhe. Kol Poh Koon aliyeambatana na wafanyabiashara mashuhuri kujifunza na kujionea fursa zilizopo nchini katika masuala ya biashara na uwekezaji. Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa anaamini kampuni za Singapore zitakazowekeza nchini zitakuwa na tija katika sekta ya mafuta na gesi asilia, kilimo, Uchukuzi pamoja na Viwanda katika kuwaletea maendeleo Watanzania. Kuhusu kuimarika kwa ushirikiano kati Tanzania na Singapore, Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa Serikali iko mstari wa mbele katika kuhakikisha inawajengea uwezo watumishi wake katika kada za uhandisi, sheria na wachumi amba...