Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Lishe Bora kwa Maisha Yote

Lishe Bora kwa Maisha Yote

Picha
Inajulikana kabisa kuwa nyumba imara hujengwa kwa mchanganyiko wa vitu vingi. Nyumba hii huonekana nzuri na yenye kupendeza wakati wote na pia haimomonyoki kirahisi wakati wa mvua au upepo mkali. Nyumba imara hujengwa kwa mchanganyiko kama wa cementi, mchanga, kokoto, nondo n.k. mchanganyiko huu huwa katika kiwango sahihi, hii ni kwamba kuna kiasi au uwiano sahihi katika mchanganyiko huu. Kimojawapo kati ya hivi kikipelea au kuwa katika kiasi pungufu basi nyumba haitakuwa imara, vilevile kimojawapo kikizidi basi nyumba haitakuwa imara pia. Hivyo nyumba ili iwe imara ni lazima mchanganyiko huu uwe katika uwiano ulio sahihi. Mpaka hapo swali linakujia, je mwili wako unajengwa na nini? je kuna uhitaji wa uwiano sahihi? Mwili wa binadamu hujengwa kwa chakula. Chakula hicho ni lazima kiwe chakula bora au mlo kamili. Mlo kamili unajumuisha makundi matano ya vyakula ambayo ni:  nafaka, mizizi na ndizi , kundi la pili:  vyakula vyenye jamii ya kunde   na vyenye asili ya wanya...