Kiwanda cha Sukari Kilombero chatumia zaidi ya Mil. 200 kufanya miradi mbalimbali ikiwepo ya elimu
Kiwanda cha Sukari cha Kilombero kimewekeza zaidi ya shilingi milioni 200 katika kipindi cha mwaka jana kutekeleza miradi mbalimbali ya kijamii katika nyanja za afya na elimu, ikiwa ni kurudisha sehemu ya pato lake kwa jamii ambapo kiwanda kinaendesha shughuli zake. Meneja wa Mfuko wa kusaidia Jamii (Kilombero Community Charitable Trust (KCCT) Mary Elizabeth alisema jana kuwa miradi iliyotekelezwa mwaka jana ni pamoja na ujenzi wa madarasa miwili katika shule za msingi Kalunga na Muungano kwa jumla ya shilingi milioni 38.5. Alisema kabla ya utekelezaji wa mradi huu, wanafunzi wa chekechea walikuwa wakisomea chini ya mti wa mwembe ambapo masomo yamekuwa yakiahirishwa mara kwa mara kutokana na mvua na wakati mwingine ilibidi kufyeka majani marefu ili kuandaa sehemu ya kusomea. Mradi mwingine uliotekelezwa ni pamoja na ujenzi wa vyoo katika shule za msingi Mang’ula and Mgudeni wenye thamani ya shilingi milioni 30. Kila choo kina mashimo sita na sehemu ya kujisaidia haja ndogo na...