Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya TRA Yabakiza Tshs. Trilioni 2.363 Kufikia Lengo Lao

TRA Yabakiza Tshs. Trilioni 2.363 Kufikia Lengo Lao

Picha
Na Ally Daud- Maelezo. Mamlaka  ya mapato Tanzania (TRA) imebakiza Tsh. Trilioni 2.363 ili kufikia lengo  waliojiwekea la kukusanya mapato ya trilioni 12.363 katika  mwaka wa fedha 2015/16, ambapo hadi sasa imekusanya kiasi cha Tsh. Trilioni 10. Akizungumza katika hafla ya uzinduzi  wa awamu ya pili ya mpango wa mafunzo kwa wafanyakazi waliopo kwenye fursa ya ajira za taasisi hiyo  Kamishina Mkuu wa TRA Bw. Alphayo Kidata alisema taasisi yake imefanikiwa kukusanya kiasi cha  sh trilioni 10 katika muda waliojiwekea na kuahidi kumalizia kiasi cha shilingi trilioni 2.363 kabla ya mwaka mpya wa fedha wa Serikali unaoanza mwezi Julai mwaka huu. “Tumejiwekea malengo ya kukusanya kiasi cha fedha cha shilingi trilioni 12.363 kwa mwaka huu wa fedha na tumefanikiwa kukusanya shilingi trilioni 10 mpaka mda huu ila tunaendelea na kutimiza lengo letu hadi kufikia July mwaka huu na tutajipanga upya mwaka ujao wa fedha kufikia malengo mapema” alisema Bw. ...