Samia: Sijawahi Kupinga Utumbuaji Majipu, Lakini Nilishauri Wakuu wa Mikoa Wazingatie Sheria Kabla ya Kumfukuza Mtu
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amewataka wakuu wa mikoa na wilaya kuzingatia sheria na kanuni za utumishi wa umma wanapotaka kuwafukuza watumishi wasio waadilifu. Alisema hajapinga kauli ya Rais John Magufuli ya kutumbua majipu kama alivyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari, hivi karibuni kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani. Samia aliyasema hayo juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha, wakati akisisitiza zoezi la kuhamisha mifugo iliyopo ndani ya Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa). Alisema wakuu wa mikoa na wilaya nchini, wanapaswa kuhakikisha wanapotaka kuwawajibisha watumishi wa umma wanafuata sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma. Aliongeza kuwa mwenye mamlaka ya kutumbua majipu ni Rais pekee, kwa sababu anateua, anaajiri na kufukuza kwa hiyo viongozi wengine wakiwamo wakuu wa mikoa na wa wilaya wafuate taratibu. “Rais pekee ndiye mwenye mamlaka ya kuteua, kutengua na kuajiri lakini sijapinga utumbuaji majipu, bali nasis...