Wabunge Wampa Makavu Waziri Kitwanga Aliyetumbuliwa Jipu Kwa Ulevi
Siku moja baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga kutimuliwa nafasi hiyo kwa ulevi, wabunge na wasomi wameendelea kumbana zaidi wakisema hatua hiyo ya Rais imechelewa. Wapinzani wamekuwa wakimtaka Rais amuondoe kwenye nafasi hiyo kutokana na kuhusishwa na Kampuni ya Infosys ambayo ilitoa ushauri kwa Kampuni ya Lugumi Enterprises iliyopewa zabuni ya kufunga vifaa vya kuchukua alama za vidole (AFIS) katika vituo vya polisi. Wakati wasomi wakisema hayo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema uamuzi huo ulikuwa sahihi na swali ambalo Kitwanga hakulijibu vizuri kutokana na hali ya ulevi, litapaswa kujibiwa upya baada ya wabunge kuomba mwongozo wa swali hilo. Majaliwa alisema Rais ametengua uteuzi wa Kitwanga kuanzia juzi baada ya kuonekana amelewa wakati wa kazi. “Na hili lilibainika pale alipokuwa akijibu maswali ya wizara yake...,” alisema Majaliwa. Alisema uamuzi wa Rais Magufuli umefuata kanuni za utumishi wa umma ambazo zinakataza mtumishi kulewa akiw...