Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya HATIMAYE Waziri Charles Kitwanga Afunguka na Kuikana Kampuni ya LUGUMI...Asema Haya

HATIMAYE Waziri Charles Kitwanga Afunguka na Kuikana Kampuni ya LUGUMI...Asema Haya

Picha
Wakati sakata la Kampuni ya Lugumi kudaiwa kushindwa kutekeleza mradi wa utambuzi wa vidole kwenye vituo vya polisi likianza kudaliwa  na  Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga amesema hana uhusiano wowote na kampuni hiyo kama watu wanavyodai.  Kitwanga ambaye alihusishwa na Lugumi kupitia kampuni ya Infosys iliyodaiwa kwamba kiongozi huyo ni mmoja wa wanahisa wakati akiwa mfanyakazi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ameeleza kuwa hahusiki na wala halijui suala la Lugumi.  Infosys ambayo imekanusha kuhusika katika sakata hilo imedaiwa kuwa iliisaidia kampuni ya Lugumi kupata vifaa kutoka kampuni ya Dell ya Marekani ili viweze kufungwa kwenye vituo vya polisi.  Jana Kitwanga alisema anashangazwa jinsi anavyohusishwa kwa maelezo kuwa wakati tukio hilo likitokea mwaka 2011, yeye hakuwa waziri wa wizara hiyo.  “Inanishangaza sana sihusiki na wala silijui hili suala la Lugumi. Wakati linatokea s...