Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya YANGA YASONGA MBELE KLABU BINGWA AFRIKA

YANGA YASONGA MBELE KLABU BINGWA AFRIKA, SASA KUKUTANA NA TIMU YA ZAMANI YA NIYONZIMA

Picha
Yanga imefanikiwa kuiondosha timun ya Cercle de Joachim ya Mauritius kwa jumla ya bao 3-0 baada ya leo kuichapa kwa bao 2-0 kwenye mchezo wa marudiano uliochezwa kwenye uwanja wa taifa. Amis Tambwe alikuwa wa kwanza kuipa Yanga bao la kuongoza dakika ya 4 kipindi cha kwanza kabla ya Thabani Kamuso kupasia kamba dakika ya 55 kipindi cha pili na kuipa Yanga ushindi huo wa michuano ya kombe la klabu bingwa Afrika. Ushindi huo unaipeleka Yanga kwenye hatua ya pili ya michuano ya ligi ya mabingwa Afrika ambapo itakutana na APR ya Rwanda katika hatua inayofuata. Unachostahili kujua Malimi Busungu, Geofrey Mwashiuya na Mwinyi Haji leo walikuwa wanacheza mchezo wa klabu bingwa barani Afrika kwa mara ya kwanza. Yanga imefanikiwa kushinda michezo miwili ya hatua ya awali kwenye michuano hiyo dhidi ya Cercle de Joachim. Mchezo wa kwanza Yanga ilishinda kwa bao 1-0 ugenini kabla ya leo kushinda kwa bao 2-0 kwenye uwanja wa taifa. Yanga inakutana kwenye raundi ya pili kwenye michuano ya Afri...