UCL: Madrid fainali ya 14, Atletico fainali 2 walizocheza zote ziliisha vibaya – hizi hapa takwimu 14 unazotakiwa kuzifahamu
Hatimaye michuano ya kombe la mabingwa wa ulaya inaelekea ukingoni kwa fainali itakayowakutanisha wababe wa jiji la Madrid – Real Madrid vs Atletico ndani ya Jiji la Milan. Kuelekea mchezo fainali tuanze kupata countdown ya matukio/takwimu yaliyotokea kuanzia kwenye hatua ya makundi mpaka nusu fainali kuelekea fainali. 1. Real Madrid wamefika kwenye fainali ya michuano ya ulaya/ChampionsLeague mara ya 14 sasa, mara nyingi zaidi ya timu yoyote. 2. Hii itakuwa mara ya 3 katika kipindi cha miaka minne ambapo fainali ya Champio League inachezwa na timu kutoka kwenye taifa moja. 3. Real Madrid wameshinda mechi zote 6 walizocheza katika uwanja wao wa nyumbani msimu huu wa Champions league – wakipata clean sheet mechi zote kwa maana ya kutoruhusu wavu wao kuguswa. 4. Cristiano Ronaldo amecheza mechi ya 17 ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya – rekodi anayoshea na Xabi Alonso. 5. Sergio Aguero amefeli kufunga ...