Silaha za biolojiki za Daesh zakamatwa nchini Morocco
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Morocco imesema kuwa, mada zilizokamatwa hivi karibuni kutoka katika kikundi kimoja chenye mfungamano na genge la kitakfiri la Daesh katika mji wa al Jadidah, ni mada za biolojiki.Wizara ya Mambo ya Ndani ya Morocco jana Alkhamisi ilitoa taarifa na kusema kuwa, wafuasi wa kundi hilo la kigaidi waliotiwa mbaroni hivi karibuni nchini Morocco wamekiri kuwa, mada hizo hatari sana zilikusudiwa kutumiwa kwenye operesheni za kigaidi ndani ya nchi hiyo.Kukamatwa mada hizo hatari za biolojiki kunaonesha kuweko mbinu mpya ya makundi ya kigaidi yenye mfungamano na Daesh katika kutenda uhalifu na jinai kwenye maeneo tofauti duniani.Wizara ya Mambo ya Nje ya Morocco imesema kuwa, wafuasi wa kundi hilo la kigaidi waliotiwa mbaroni wamekabidhiwa kwa idara ya mahakama ya nchi hiyo ili wapandishwe kizimbani.