Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya BAYERN YATULIZWA VICENTE CALDERON

BAYERN YATULIZWA VICENTE CALDERON

Picha
Goli pekee la Saul Niguez limeiweka Atletico Madrid kwenye nafasi nzuri ya nusu fainali ya Champions League dhidi ya miamba ya soka la Ujerumani Bayern Munich. Niguez akiipangua ngome ya ulinzi ya Bayern kabla ya kuukunja mpira kwenye kona ya goli na kuipa timu yake ushindi mwembamba wa mechi ya kwanza kabla ya kurudiana kwenye game ya pili itakayopigwa Ujerumani. Bayern walitawala kipindi chote cha pili, shuti la David Alaba akiwa umbali wa mita 35 liligonga post ya juu ya lango la Atletico kabla ya golikipa wa Atletico kufanya kazi ya ziada kuokoa shuti jingine la Arturo Vidal. Atletico walifanya shambulizi la kushtukiza (counter attack) lakini shuti la Torres liligonga mwamba. Timu hizo zitakutana tena kwenye mchezo wa marudiano kwenye dimba la  Allianz Arena Jumatano ya juma lijalo kuamua nani atakutana na Manchester City au Real Madrid kwenye mchezo wa fainali utakaopigwa May 28. Takwimu muhimu Atletico wameshinda michezo 13 kati ya michezo 17 ya Champions League ...