Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya MAUMIVU WAKATI WA KUKOJOA

MAUMIVU WAKATI WA KUKOJOA

Maumivu wakati wa kukojaoa ni hali inayotokea kwa watu wengi ikisababishwa na magonjwa mbalimbali. Maumivu wakati wa kukojoa hujulikana kwa kitaalamu kama dysuria. Kati ya sababu kuu za maumivu wakati wa kukojoa ni maambukizi ya mfumo wa mkojo (Urinary tract Infection – UTI) hasa kwa wanawake na magonjwa ya zinaa. Namna Maumivu Wakati Wa Kukojoa Yanavyotokea Maumivu haya hutokana na kuchubuka kwa njia ya mkojo. Maumivu huwa yanakuwa ya kuungua wakati mkojo unatoka. Yanaweza kuwa wakati wote unakojoa, mwanzoni au mwishoni mwa kukojoa. Pia yanaweza kuambatana na dalili kama homa, kuokwa na usaha au uchafu sehemu za siri, kutokwa mkojo wenye damu damu na maumivu chini ya kitovu. Maumivu haya hutegemea na chanzo cha ugonjwa unaoleta dalili hii. Baadhi ya sababu za maumivu wakati wa kukojoa ni: Maambukizi ya Njia ya Mkojo (Urinary Tract Infection – UTI) Ugonjwa huu huleta maumivu kama ya kuungua kwenye njia ya mokojo. Pia maumivu yanaweza kufika mpaka chini ya kitovu wakat...