Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Waziri Mkuu: Serikali Itahakikisha Inaendelea Kulinda Rasilimali Za Nchi Ikiwemo Urithi Wa Dunia

Waziri Mkuu: Serikali Itahakikisha Inaendelea Kulinda Rasilimali Za Nchi Ikiwemo Urithi Wa Dunia

Picha
SERIKALI ya awamu ya tano  imesema kuwa itaendeleza jitihada za kutunza na kulinda urithi wa dunia ikiwemo kutoa elimu kwa wananchi wanaoishi maeneo ya uhifadhi ili watanzania wote waweze kunufaikana rasilimali za nchi . Hayo yalisemwa na  waziri mkuu Kassim Majaliwa alipokuwa akifungua mkutano wa kulinda urithi wa dunia wa Afrika kama nyenzo ya maendeleo endelevu unaoendelea jijini Arusha Majaliwa alisema kuwa rasilimali zilizopo ni za watanzania na ili kuhakikisha kuwa wananufaika nazo serikali itahakikisha  inatunza na kulinda uhifadhi ili yawe endelevu na  kusaidia vizazi vijavyo. Alisema kuwa Tanzania ni moja ya nchi tajiri yenye urithi na hivyo ili kuhakikisha kuwa wananchi wananufaika haswa waishio maeneo ya uhifadhi serikali itatoa elimu ya kutosha ili waepuke kuchangia uharibifu wa mazingira unaotokea kwenye hifadhi za taifa .   “Rasilimali hizi ni zetu na hivyo hata wanaoishi maeneo ya hifadhi watusaidie kwa wale wanaoingilia na kuharibu...