Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya 12 Wakamatwa Wakituhumiwa Kuhusika na Mauaji ya Watu 7 Jijini Mwanza

12 Wakamatwa Wakituhumiwa Kuhusika na Mauaji ya Watu 7 Jijini Mwanza

Picha
Siku chache baada ya watu saba wa familia moja kuuawa kwa mapanga wilayani Sengerema mkoani Mwanza, polisi wamefanikiwa kuwatia mbaroni watu 12 kwa tuhuma za mauaji hayo huku mmojawapo akikamatwa kwa mganga wa kienyeji alikokuwa akijitibu. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema hadi jana upelelezi wa tukio hilo lililozua hofu kwa wakazi wa Kijiji cha Sima unaendelea na tayari watuhumiwa 12 wamekamatwa. “Hakuna jiwe litakalobaki bila kugeuzwa katika upelelezi wa jambo hili, tutawasaka na kuwakamata wote waliohusika kwa njia moja au nyingine na mauaji haya ya kinyama,”  alisema Msangi. Habari zilizopatikana kutoka kwa mtu wa karibu na familia ya marehemu Zakaria Mbata iliyopoteza mama na watoto watatu katika tukio hilo, zinaeleza kuwa wauaji walilenga kupora fedha zilizohifadhiwa kwenye mtandao wa simu. Pia, chanzo kimoja cha habari kilisema kuwa polisi walimkamata mmoja wa watuhumiwa hao akiwa kwa mganga wa kienyeji alikokuwa akijitibu jeraha alilop...