Tanzania ya Rais Magufuli na Kenya ya Rais Kenyata ziko Katika Vita Baridi?
Ni ukweli kuwa uhusiano wetu na Kenya haujawahi kuwa wa "mahaba" (tukitumia msemo wa Lowassa). Tumekuwa tukivumiliana kwa maslahi ya kiuchumi tangu enzi za mwalimu. Hata hivyo tangu awamu ya tano ianze uhusiano wetu na Kenya unatia mashaka na ni vema tukaongelea jambo hili objectively. Mambo yalianza na Magufuli kuchaguliwa kuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM. Ikaelezwa viongozi wa serikali ya Kenya walipata hofu kwa vile Magufuli ana urafiki na kiongozi wa upinzani. Likaja suala la njia ya Bomba la Mafuta. Magufuli akaongea na Mseveni na kukawa na uwezekano mkubwa kuwa Uganda itachagua njia ya Tanzania badala ya Kenya. Suala hili halikuifurahisha Kenya hata kidogo. Kwa sababu ya ushindani wa njia ya bomba la mafuta wakati fulani waziri mmoja wa kenya na maafisa wake walizuiliwa uwanja wa ndege Tanga. Jambo jingine la kuchekesha ambalo wakenya waliandika ni wakati wa mkutano wa marais wa EA ambapo Magufuli aliongea ki-luo mbele ya Kenyatta. Media ya Kenya ikac...