Alinipenda Sana Kabla Hajapata Kazi, Sasa Kapata Kazi Ananiona Bwege
Najuta ni kiherehere cha moyo wangu kukupenda,kukuthamini na jukujali. Naombeni msaada,ni mpenzi wangu yapata 1&half year katika mahusiano ni binti ambaye tulifahamiana nae siku moja alipokuja na mama yake mdogo ofisini kwangu kupata huduma, huyu mama yake mdogo ni mtu ninaefahamiana nae hivyo basi akaona haina budi kunitambulisha kwa mwanae nami nikaona ni vizuri kuanzia hapo binti yule alianza kunizoea na kuonesha dalili zote za kunitaka hata baadhi ya siku hufunga safari na kuja kunisalimia. nami sikua na hiyana huwa sipendi kumkwaza mtu nikawa nampa ushirikiano tu mzur. kutokana na ubize wa kazi yangu muda wa story huwa sina nikamwambia kama hutojali uwe unakuja saa 12jioni muda ambao nipo off ila sijui kama mama yako mdogo atakubali akasema hilo halina shida nikimwambia nakuja kwako hawezi kunikatalia kiukweli hilo jibu lake lilinipa ulakini!! Basi jioni tukawa tunaenda sehemu ya utulivu tunapiga story sana tunapata chakula then tunaondoka tuliendelea hivyo kwa mud...