Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya SUMATRA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI MADEREVA NA MAKONDAKTA WOTE WATAKAOWATOZA ABIRIA NAULI KUBWA TOFAUTI NA ZILIZOPANGWA

SUMATRA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI MADEREVA NA MAKONDAKTA WOTE WATAKAOWATOZA ABIRIA NAULI KUBWA TOFAUTI NA ZILIZOPANGWA

Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi Usafiri wa Majini na Nchi Kavu  (SUMATRA) Mkoa wa Kilimanjaro  kuwafikisha mahakamani madereva wote na makondakta wanaowatoza abiria nauli kubwa tofauti na zilizopangwa na ofisi hiyo. Hayo yamesemwa leo na Kaimu Afisa Mfawidhi Bw.Tadei Mwita alipokuwa akijibu kero ya mkazi wa mkoa huo kwa njia ya simu iliyotolewa na Gazeti  la Mwananchi Machi 04, mwaka huu,iliyozungumzia  daladala zinazofanya safari zake kati ya Moshi Mjini - Himo kuwatoza nauli ya shillingi 1000 abiria wanaoshuka maeneo ya Kiboriloni, Sango Pumuani na Kawawa road tofauti na nauli iliyopangwa na SUMATRA katika vituo hivyo. “Kuanzia wiki ijayo wadau wote  watakao kuja kuomba leseni kwa ajili ya usafirishaji wa abiria ndani ya mkoa huu watahitajika kuonyesha nauli watakazo toza abiria katika vituo vya katikati kabla ya kufika kituo cha mwisho cha safari zao,”alisema Bw.Mwita.  Bw.Mwita alisema hivi sasa SUMATRA Mkoa wa Kilimanjaro  imeanzi...