Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Tanesco Mkoa Wa Pwani Yamakamata Mmiliki Wa Yadi Ya Magari Kwa Wizi Wa Umeme

Tanesco Mkoa Wa Pwani Yamakamata Mmiliki Wa Yadi Ya Magari Kwa Wizi Wa Umeme

Picha
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Mkoa wa Pwani limemkamata mmoja wa wamiliki wa eneo la maegesho ya magari la White Star, Munira Mbowe akidaiwa kujiunganishia umeme kinyume cha sheria. Mbowe ambaye ni mmiliki wa eneo hilo lililopo Kiluvya kwa Komba nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, alikamatwa jana baada ya kufanyika msako wa kushtukiza kwa watu wanaodaiwa kujiunganishia umeme kinyume cha sheria. Inadaiwa kuwa Mbowe amelisababishia shirika hilo hasara ya Sh50 milioni. Akizungumza kwenye eneo hilo, Ofisa Usalama wa Tanesco Mkoa wa Pwani, Henry Byarugaba alidai kuwa baada ya kufanya ukaguzi waligundua umeme uliokuwa ukitumika katika eneo hilo haukuunganishwa na Tanesco. “Tumekuwa tukibuni mbinu mpya kila kukicha ya kuwatia mbaroni wateja wetu wanaotuhujumu na leo (jana), tumembana huyu anayedaiwa ni mmiliki wa yard hii ya White Star baada ya kukuta anatumia umeme wa wizi uliounganishwa katika njia tatu,”  alidai Byarugaba. Alisema tayari wameshamfikisha Kituo ...