Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Akabidhiwa zana ya ‘Kisukuma’ Kukabili MAJIPU......Pia Kapewa Jina Jipya ambalo ni Masanja Mkusanyaji
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amepewa jina jipya la Kisukuma na kukabidhiwa zana nyingine muhimu katika vita ya kupambana na ufisadi nchini maarufu kwa jina la kutumbua majipu. Kuanzia juzi, Waziri Mkuu Majaliwa atakuwa akifahamika kwa jina lingine la Masanja, alilopewa na Wazee wa Kisukuma wa Lamadi wilayani Busega katika mkoa wa Simiyu. Kabla ya kuwahutubia maelfu ya wakazi wa Lamadi juzi jioni, wazee hao walimvisha Waziri Mkuu vazi la kijadi la Kisukuma akiwa katika kigoda, wakamkabidhi usinga, ng’ombe wawili na mkuki ambao walimueleza kuwa kazi yake ni kuendeleza vita ya ufisadi kwa kuutumia kutumbua majipu. “Tunakukabidhi usinga na huu mkuki utumike kutumbua majipu kwa sababu kazi hii unaifanya vizuri hadi sasa, kwa hiyo uendelee kutumbua majipu. Na kwa kuanzia sasa, tunakupa jina la kwetu, kwa sababu wewe ni kijana wetu, utaitwa Masanja,” alisema Mchele Malale kwa niaba ya wazee wenzake. Kwa mujibu wa wenyeji, jina la Masanja lina maana ya kuingia kokote, hali...