Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Upinzani Burundi Wataka AU

Upinzani Burundi Wataka AU,EU wasishiriki mazungumzo ya kutafuta amani

Picha
Mzunguko wa kwanza wa mazungumzo ya Burundi umemalizika, huku kukiwa na mvutano kuhusu kualikwa kwa chama cha CNARED, kinachojumuisha wanasiasa wanaoishi nje ya Burundi.  Msuluhishi wa mgogoro huo, Rais mstaafu wa Tanzania, Benjamin Mkapa alisema mzunguko wa kwanza ulijikita zaidi katika ‘mazungumzo binafsi’ na Serikali.  Alisema mzunguko wa pili utaanza mwishoni mwa mwezi ujao na kwamba atakutana na vikundi ambavyo havikuhudhuria mzunguko huo, akiamini vitakuwa na mchango wenye masilahi.  Burundi imekuwa kwenye mgogoro huo baada ya uchaguzi uliopita na zaidi ya watu 450 wameuawa tangu Rais Pierre Nkurunziza alipogombea kipindi cha tatu cha urais na kushinda.  Wapinzani wake wanadai kugombea kwake kumevunja Katiba inayotamka vipindi vya urais ni viwili. Mzunguko wa kwanza wa mazungumzo hayo ulianza mwishoni mwa wiki jijini Arusha, baada ya majadaliano ya mwaka jana kabla ya Mkapa kuteuliwa, yaliyofanyika kwa nyakati tofauti katika nchi za Burundi na...