Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Freeman Mbowe: Nawaletea Katibu Mkuu Makini Wakuvaa Viatu vya Dr Slaa

Freeman Mbowe: Nawaletea Katibu Mkuu Makini Wakuvaa Viatu vya Dr Slaa

Picha
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amevunja ukimya na kusema atawasilisha jina makini la mrithi wa nafasi ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa. Akizungumza na MTANZANIA mjini hapa jana, baada ya kumalizika kikao cha kwanza cha Kamati Kuu, Mbowe alisema sifa za kiongozi anayepaswa kushika wadhifa huo zinafahamika. Alisema wajumbe na wanachama wa Chadema watarajie kumpokea mtu makini ambaye jina lake atalipendekeza kisha kupigiwa kura na wajumbe wa Baraza Kuu kesho. “Sifa za Katibu Mkuu zinajulikana, nawaomba wanachama na wajumbe kutulia, jina watakutana nalo ukumbuni muda ukifika… nina imani litakuwa jina la mtu makini,” alisema. Mbowe alisema chama hicho kinakutana kwa mara ya kwanza tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa Rais mwaka jana, hivyo wana mambo mengi ya kujadili, ikiwa ni pamoja na kupanga mikakati mipya ya kuwafikia wafuasi wao. Katika hatua nyingine, chama hicho kimesema kitamtambulisha Kat...